Watumishi wa Ataba mbili tukufu watoa taazia kwa Imamu wa Zama (a.f) katika kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu wa nne mtakasifu ambaye ni Imamu Sajaad (a.s).

Maoni katika picha
Juma Nne (25 Muharam 1439h) sawa na (16 Oktoba 2017m) baada ya Adhuhuri, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walifanya matembezi ya maombolezo kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu wa nne, ambaye ni pambo la waabudio na mmbora wa wasujudio Imamu Ali bun Hussein (a.s), matembezi yalianzia katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wakaenda hadi katika kaburi la Imamu Hussein (a.s), huku wanasoma kaswida za huzuni, zilizo sababisha kuenea huzuni kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), halafu wakafanya majlis ya maombolezo katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s).

Imamu Sajaad (a.s) ni; Ali bun Hussein bun Ali bun Abutwalib (a.s), ni Imamu wa nne miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), na jina lake la kuniya ni Abuu Hassan, huku jina la sifa ambalo ni mashuri zaidi ni; Zainul Aabidina na Sajaad. Mama yake anaitwa Shahazanan bint Yazdajrad. Amirulmu-uminina (a.s) alimpa uongozi katika miji ya Mashariki bwana Harith bun Jaabir Hanafiy, naye bwana Harith akamtumia Amirulmu-uminina mabinti wawili, Akamuozesha mwanaye Hussein (a.s) bint mmoja ambaye ni Shahazanan, aliye mzalia Zainul-Aabidina (pambo la waabudio) (a.s), na bint wa pili akamuozesha kwa Muhammad bun Abu Bakari naye akamzalia Kassim.

Imamu (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina mwaka wa (38h) na aliishi na babu yake Amirulmu-uminina miaka miwili, na akaishi na Ammi yake Hassan (a.s) miaka kumi, na akaishi na baba yake baada ya kufariki kwa ammi yake miaka kumi na moja, na baada ya kufariki baba yake aliishi miaka thelathini na nne, mwaka wa (95) hijiriyya, aliuawa kwa sumu katika mji wa Madina akiwa na umri wa miaka hamsini na saba, alichukua madaraka rasmi ya Uimamu baada ya kufariki kwa baba yake Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Twafu, alishuhudia kuuawa kwa watu wa familia yake katika aridhi ya Karbala. Amani imuendee Hussein na Ali bun Hussein na watoto wa Hussein na maswahaba wa Hussein.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: