Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Juma Nne (26 Muharam 1439h) sawa na (17 Oktoba 2017m), wameanza kazi ya kusafisha mji wa Karbala na mitaa yake, kwa ajili ya kujiandaa kupokea watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq.
Kundi la watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi hii ili kuwapunguzia mzigo wakazi wa Karbala na kuufanya mji uwe na muonekano mzuri kwa wageni, hii sio mara ya kwanza kufanya shughuli kama hizi, hakika wamesha fanya kazi mbalimbali katika matukio tofauti.
Kiongozi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, Ustadh Riyadh Khadhir Hassan amezungumzia swala hili kua: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa kitengo cha utumishi Haji Khalil Hanun, wote kwa pamoja wameonyesha umuhimu wa kufanya usafi katika mji wa zamani, wahudumu wa idara ya usafi toka saa moja asubuhi wameanza kufanya kazi ya usafi kwa ajili ya kujiandaa na mapokezi ya watu wanaokuja kufanya ziara ya arubaini ya Imamu Hussein (a.s), walielekea katika mji wa zamani na kuanza kutoa taka katika barabara kubwa na ndogo, kwa kuanzia na barabara ya mkono wa kulia na wa kushoto ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakaendelea na usafi hadi katika barabara ya Maitham Tamaar, kazi hii itaendelea kufanyika kila siku hadi mwisho wa ziara ya Arubainiyya”.
Akaongeza kua: “Lengo letu ni kuuweka mji katika hali ya usafi na muonekano mzuri, hususan katika siku hizi ambazo tunapokea watu kila siku wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.