Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ushiriki wake wa wiki ya kitamaduni (kongamano la msimu wa Ashura) linalo fanyika katika mji wa Takab huko Iran chini ya usimamizi wa Atabatu Husseiniyya, sambamba na hilo; wameshiriki maonyesho yanayo fanywa pembozoni mwa kongamano hilo kwa kuweka vitu vya tabaruku.
Vitu walivyo onyesha vimegusa hisia za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na vinawakilisha msimamo wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) walio onyesha katika vita ya Twafu, ambavyo ni: Bendera mbili, moja imeandikwa (Yaa Hussein) na nyingine imeandikwa (Yaa qamaru baniy Hashin), miito ya uaminifu na ujasiri, pia kulikua na vifaa vingine, kama vile; panga, ngao, upinde na kiriba cha maji, vitu ambavyo vina ashiria ushujaa aliokua nao Abbasi (a.s), mtu mwenye sifa ya pekee ya unyweshelezaji wa maji na mbeba bendera ya kaka yake Imamu Hussein (a.s).
Miongoni mwa vitu vilivyo kuwepo pia ni kitambaa kilicho kua katika moja ya milango ya haram tukufu, ambapo watu wengi wamefanya tabaruku kwa kitambaa hicho, na wakaomba kumuona Imamu wa zama, Imamu Mahdi (a.f) na kushiriki pamoja naye katika kulipa kisasi kwa kuuawa kwa babu yake Imamu Hussein (a.s).