Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuzitunza kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu chatoa picha (750) za nakala kale ambazo ni nadra..

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuzitunza kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanikiwa kupiga picha nakala kale kutoka katika maktaba ya Sayyid Hakiim katika mji mtukufu wa Najafu, hii ni miongoni mwa taratibu kilizo jiwekea za kuenzi turathi za kiislamu, hususan turathi za Ahlulbait (a.s), na hili ndio jukumu lao la msingi, kupiga picha nakala kale na kuziandaa kwa ajili ya kutumiwa na wasomi pamoja na watafiti, ndio maana kituo hiki kimepiga picha kundi jipya la nakala kale zilizo hifadhiwa katika maktaba ya Sayyid Hakiim chini ya wataalamu wake.

Ustadh Swalahu Mahdi Abdulwahaab, mkuu wa kituo cha upigaji picha na utunzaji wa nakala kale chini ya Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tulikubaliana na katibu mkuu wa maktaba ya Sayyid Hakiim iliyopo katika mji mtukufu wa Najafu Sayyid Jawaad Hakiim kuhusu kupiga picha baadhi ya nakala kale zilizopo katika maktaba hiyo, hadi sasa tumesha piga picha zaidi ya (750) za nakala kale muhimu, na tumeziingiza katika benk (orodha) ya nakala kale tulizo zipiga picha na kuzitunza kutoka kila sehemu ya dunia, ambapo zinakaribia kufika laki tatu. Pamoja na upigaji wa picha, pia tumekubaliana kubadilisha kutuko aina ya utunzaji wa kizamani na kutumia mbinu ya kisasa ambayo ni mbinu ya namba na ndio inayo tumika katika kituo chetu, kwa kutumia mbinu hii tayali tumesha tengeneza filamu (250), zilizo jaa nakala kale nyingi na muhimu, kila filamu ndani yake kuna nakala kale nne au tano ambazo historia yake inarudi katika karne tofauti za nyuma”.

Fahamu kua maktaba hii ni miongoni mwa maktaba muhimu, inachukuliwa kua ni mwalimu mkubwa katika mji wa Najafu kutokana na kuwepo kwa vitabu na nakala kale muhimu ndani ya maktaba hii, pamoja na zaidi ya mikanda ya filamu (250) iliyo beba zaidi ya nakala kale (700) zilizo kusanywa kutoka katika nakala kale za waarabu huko nchini Misri, kupitia kamati maalumu iliyo undwa na Ayatullah Sayyid Muhsin Hakiim wakati huo, na zimebeba urithi wa kielimu na kitamaduni ambazo zinawasaidia sana wanafunzi na wahakiki wa turathi za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: