Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na mikakati yake ya kuboresha huduma kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa, imeanza kutumia kifaa cha (Dexa Scan) katika upimaji wa mifupa.
Mkuu wa kitengo cha matibabu dokta Muhammad Shimaai amesema kua: “Uongozi wa hospitali ya Alkafeel unatilia umuhimu mkubwa wa kutumia vifaa vya kisasa katika kupima magonjwa mbalimbali, miongoni mwa vivaa hivyo ni hiki kinacho tumika katika kupima matatizo ya mifupa na kina uwezo mkubwa wa kubaini mipasuko au athari yeyote iliyopo katika mfupa, pia kinasaidia kubaini hali ya saratani baada ya matibabu ya kikemekali, vilevile kinatumika katika kupima kiwango cha mafuta katika viungo vya mwanadamu pamoja na maswala yote yanayo husu mifupa”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika kipimo hiki ni salama, athari iliyopo katika myonzi yake ni ndogo sana ukilinganisha na vipimo vingine, na majibu yake ni ya uhakika, kipimo hiki ni faraja kubwa kwa madaktari na wagonjwa”.
Akaendelea kusema kua: “Kupima mapemba matatizo ya mifupa kunamsaidia mgonjwa kuepuka tatizo la kuvunjika kwa mifupa, mtu anaweza kupima kwa kuja hospitalini kwetu au katika hospitali zingine”.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali, unaweza kutembelea toghuti yetu kwa anuani hii: www.kh.iq au piga simu kwa namba zifuatazo: 07602344444 au 07602329999.