Aliyasema haya katika hotuba ya pili ya swala ya Ijumaa (29 Muharam 1439h) sawa na (20 Oktoba 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbu wa haram ya Imamu Hussein (a.s) na kuongozwa na Shekh Abdulmahadi Karbalai, alieleza mambo mengi miongoni mwake ni:
- 1- Wote tunafahamu yaliyojiri karibuni katika uwanja wa kisiasa na kijeshi, kurudi kwa wanajeshi wa Iraq na vikosi vya muungano katika mkoa wa Karkuk na baadhi ya maeneo mengine, tunatoa pongezi kwa ushirikiano mzuri ulio onyeshwa na pande mbalimbali, ulio pelekea kufanyika zoezi hili kwa usalama na amani baina ya ndugu zetu wapenzi walio pigana bega kwa bega dhidi ya magaidi ya Daesh.
- 2- Tunasisitiza kua jambo hili haifai kabisa kusema kua upande fulani umeshinda na upande fulani umeshindwa, bali ni ushindi wa kila raia wa Iraq kwa maslahi ya taifa na sio maslahi ya mtu au kundi fulani, inatakiwa kuufanya kua mwanzo mpya wa kushikamana wananchi wote kwa pamoja na kujenga taifa lao.
- 3- Raia wa Iraq wote sawa awe Muarabu, Mkurdi, Mturkuman na wengine wanatakiwa kuishi kwa amani katika aridhi hii tukufu.
- 4- Raia wa Iraq hawana nafasi ya kujenga kesho nzuri watakayo ishi kwa amani na utulivu ispokua wafanye juhudi za pamoja kutatua matatizo yaliyo kuwepo miaka na miaka kwa kufuata misingi ya uadilifu na usawa kwa wote, na lazima kujenga kuaminiana baina yao na kuepuka mizozo ambayo husababishwa na maslahi binafsi ya watu au kundi fulani, kila palipo na tatizo yatupasa kurudi katika katiba kwani ndio maamuzi ya wananchi wengi, lazima tuiheshimu na kufuata maelekezo yake madamu haijafanyiwa marekebisho kwa mujibu wa sheria.
- 5- Tunawaomba watu wote hususan wana siasa, waweke uzalendo wa nchi yao mbele na waheshimu katiba, wajenge mapenzi na maelewano baina ya raia wa Iraq, wahakikishe wanalinda maslahi ya kila mtu bila upendeleo, wajiepushe na mambo yanayo weza kuleta mizozo na kuvunja maelewano hasa katika miji ambayo wanaishi watu wa jamii tofauti.
- 6- Tunaomba wawafanyie wepesi watu (wakimbizi) kurudi katika miji yao, na wawahakikishie usalama wa mali na nafsi zao.
- 7- Tujizuie kufanya jambo lolote linalo ashiria ubaguzi dhidi ya kundi lingine, kama vile kusambaza kipande cha video, picha, sauti au kubeba bango, kuchoma picha na mengineyo.
- 8- Tunawaomba watu wenye mamlaka kuwachukulia hatua watu watakao fanya mambo haya yanayo vunja amani na mshikamano wa wananchi wa taifa hili tukufu.
- 9- Tunaiomba serikali kuu ya Iraq ihakikishe usalama wa raia wa kikurdi sambamba na raia wengine bila upendeleo wowote, na iwahakikishie kua italinda haki zao zote kwa mujibu wa katiba.
- 10- Tunawaomba viongozi watukufu wa ndugu zetu wapenzi wakurdi, waungane pamoja na waangalie namna nzuri ya kumaliza matatizo yaliyopo kwa kushirikiana na serikali kuu chini ya muongozo wa katiba, tunatarajia kupata utatuzi adilifu utakao ridhisha pande zote.