Watu wa Basra wanatembea kwa miguu kwenda Kurbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Mkoa wa Basra ni miongoni mwa sehemu ambazo watu wake hutemea kwa miguu kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika msimu wa ziara ya Arubainiyya, kabla ya siku tatu katika mji wa Ra-asu Bishah wilaya ya Faau kusini mwa mji wa Basra, yalianza matembezi ya kuonyesha mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s), ambapo watu wanatembea kwa miguu kwenza Karbala kufanya ziara ya Arubainiyya, matembezi hayo huwa na ushiriki mkubwa wa raia wa Iraq na kutoka nchi za jirani, fahamu kua mkoa huo unapakana na Kuwait na Iran pia kuna uwanja wa ndege wa kimataifa, watu hutembea kati ya kilometa 25 hadi 30 kwa siku, kila mtu hutembea kutokana na uwezo wake.

Matembezi hayo huambatana na kundi la wahudumu na wanausalama, pia kuna vikundi (mawakibu) za husseiniyya njia nzima, ambao wanatoa huduma za chakula na vinywaji pamoja na kila kitu anacho hitaji mtembeaji, mahema yamejengwa njia nzima watu wamefungua milango ya nyumba zao kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru watukufu (huduma zote zinatolewa bure).

Idadi ya mawakibu (vikundi) vinavyo toa huduma kwa watembea kwa miguu, kwa mujubu wa ofisi ya mkoa wa Barsa ni zaidi ya (1750) zilizo sajiliwa rasmi, babo kuna husseiniyya nyingi pamoja na nyumba za watu binafsi ambazo zinatoa huduma bila kusajiliwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: