Shahidi asulibiwa mwezi pili Safar, Kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Zaidu bun Ali (a.s)..

Malalo yake tukufu
Mwezi wa Safar unamatukio mengi ya kuhuzunisha na kuumiza yalio wapata watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Mwezi pili Safar mwaka wa (122h), aliuawa kishahidi Abul-Hussein Zaidu Shahid bun Imamu Ali Sajjaad bun Abu Abdillahi Hussein bun Amirulmu-Uminina Imamu Ali bun Abuutwalib (a.s).

KUZALIWA KWAKE:

Alizaliwa mwaka wa (57) hijiriyya, na akalelewa katika nyumba ya utume, na akakulia mikononi mwa baba yake Imamu Zainul-Aabidin (a.s), akasoma matukufu ya baba yake na akapata elimu bora kutoka kwa baba yake, baadhi ya riwaya zinasema kua Mtume (s.a.w.w) ndiye aliye mpa jina hili na akabashiri kuzaliwa kwake, jina lake la sifa (laqabu) anaitwa (Haliful-Qur’an), Abuu Jaarud anasema kua: Nilienda Madina, kila niliye muuliza kuhusu Zaidi alisema! Yule Haliful-Qur’an, yule ni pambo la msikiti kutokana na wingi wa swala zake.

ELIMU YAKE:

Alifikia kiwango cha juu kabisa cha elimu, hakika (a.s) alikua mwanachuoni mkubwa katika zama zake, alisoma kwa baba yake Imamu Zainul-Aabidin (a.s) na kwa maimamu wawili watakasifu, Imamu Baaqir na Swaadiq (a.s), hakika alisoma maarifa mema kutoka kwa maimamu hao watakatifu, wanachuoni na wataalamu wote wa zama zake walitambua ukubwa wa elimu yake, ushahidi mzuri wa hilo ni pale Imamu Swaadiq (a.s) alipo sema: (Hakika Zaidi alikua Aalim na muaminifu) alikua mcha Mungu, Faqihi Mnyenyekevu na Shujaa, alitoka na upanga (siraha) kwa ajili ya kuamrisha mema na kukataza mabaya na kulipa kisasi cha babu yake Hussein (a.s), maneno yake yalikua yanafanana na maneno ya babu yake Ali bun Abutwalib (a.s) kwa balagha na ufasaha.

MAPAMBANO YAKE NA KUUAWA KWAKE KISHAHIDI:

Vita ilikua kali sana toka siku ya Juma Tano ya Mwezi wa Safar (122h) hadi siku ya Ijumaa, vita kali hiyo ilipiganwa katika mji wa kufa kwa muda wa siku tatu, jioni ya siku ya Alkhamisi, Zaidi na wapiganaji wake waliwavamia maadui walio kua wakiongozwa na Abbasi bun Saidi aliye kua kamanda wa mji wa Kufa pamoja na wapiganaji wa Sham, akawapiga hadi akawatoa katika eneo la Sabkha, akaendelea kuwashambulia hadi kwa baniy Salim, akaendelea kuwashambulia na kuwatoa nje zaidi, kamanda wa jeshi la Zaidi katika vita hii alikua anaitwa Abduswamad bun Abu Maalik bun Masruuh bun baniy Saadi, Jeshi la Abbasi halikuweza kuhimili mapigano dhidi ya jeshi la Zaidi, Abbasi akatuma ujumbe kwa Yusufu akaomba aongezewe wapikanaji, akaongezewa vikosi vya warusha mishale vikiongozwa na Suleimaan bun Kisaan Kalbiy, Zaidi akaendelea kupigana nao, akauliwa Muawiya bun Is-haqa baada ya kua amesha uliwa Nasoro bun Khuzaima hao ni wapiganaji muhimu katika jeshi la Zaidi, haukipita muda mrefu na Zaidi akachomwa mkuki katika paji la uso wake upande wa kushoto, ukaingia hadi kwenye ubongo, akaenda katika nyumba za wauza nyama akiwa na maumivu makali sana. Akapelekewa daktari anaye itwa (Sufiyan aliye kua mtumishi wa bani Dawaas) wakamuomba amchomoe mkuki uliokua umemuingia usoni, daktari akasema: Hakika tukichomoa huu mkiki kichwani kwako utakufa. Akasema: (Ni juu yangu kufikwa na kifo, ndipo wakaanza kuchomoa mkuki ule kichwani na baada ya kuutoa hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, watu wake wakamchukua na kwenda kumzika katikati ya mto ili kuficha mwili wake maadui wasije kuuchukua na kuusulubu, lakini kuna mtu mmoja akatoa siri hiyo kwa Yusufu bun Omari wakaenda kuutoa mwili huo mtakatifu na wakaanza kuusulubu, wakakata kichwa chake na wakakipeleka kwa Hisham bun Abdulmalik, naye akakipeleka Madina na kukitungika juu ya kaburi la Mtume (s.a.w.w) kisha wakakipeleka Misri, huko mmoja kati ya wafuasi wa Zaidi akakiiba na kwenda kukizika.

Imamu Swaadiq (a.s) alipo pata taarifa ya kuuawa kwa Zaidi (r.a) alilia sana na akasema: “Innaa lilaahi wa Innaa ilaihi raajiuun, Natarajia Ammi yangu atapata malipo mema kwa Mwenyezi Mungu, hakika alikua Ammi bora zaidi, hakika alikua mtu muhimu kwetu duniani na akhera, hakika amekufa shahidi kama mashahidi walio uawa pamoja na Mtume (s.a.w.w) na Ali, Hassan na Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: