Kikosi cha Abbasi (a.s) cha jiandaa kwenda kukomboa mji wa Qaaimu na chasuburi tangazo la kuanza rasmi kwa mapambano..

Maoni katika picha
Maandalizi makubwa baada ya yale yaliyofanyika katika vita ya kukomboa mji wa Bashiri mwaka jana (2016m), vikosi vya Abbasi (a.s) vimewasili katika maeneo ya mji wa Qaaimu uliopo katika mkoa wa Anbaar, kwa ajili ya kushiriki katika vita ya kukomboa mji huo kutoka mikononi mwa Daesh, na ndio mji wa mwisho uliobakia mikononi mwao katika nchi ya Iraq, inatarajiwa vita hii kua ndio ya mwisho baada ya kudumu vita hizi kwa miaka mitatu na mwiezi minne.

Maandalizi haya yametanguliwa na upelelezi wa kina ulio fanywa na viongozi wa kikosi hiki pamoja na vikao kadhaa vilivyo fanywa na viongozi wa jeshi sambamba na mazoezi ya kijeshi ya kikosi pekeyake na ya pamoja na vikosi vingine vya Hashdi Sha’abi.

Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wameubainishia mtandao wa kimataifa Alkafeel ukubwa wa maandalizi hayo kama ifuatavyo:-

  • Ø Kikosi cha deraya kikiwa na brugedi nne.
  • Ø Kikosi cha watembea kwa miguu, kikiwa na wapiganaji (1000) miongoni mwao kuna brugedi ya wapiganaji wenye hasira.
  • Ø Kikosi cha uhandisi.
  • Ø Kikosi cha mitambo ya elektronik (waangalizi na watumiaji wa ndege za upelelezi zisizo kua na rubani).
  • Ø Kikosi cha vifaru na mabomu.
  • Ø Kikosi cha mikakati.
  • Ø Kikosi cha walenga shabaha.
  • Ø Kikosi cha kuvunja ngome (ngao).

Pamoja na vikosi vingine vya usaidizi.

Viongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) wakabainisha kua; vita hii haita athiri katika utendaji wa wapiganaji wake waliopo katika miji mingine iliyo kombolewa na wale waliopo katika mipaka ya mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: