Kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika nchi ya Iraq na ulimwengu wa kiislamu, kilichopo chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimetoa maelekezo kwa viongozi wa vikundi vya Husseiniyya vinavyo toa huduma katika msimu huu wa ziara ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s), ili kuweka mazingira mazuri yatakayo endana na utukufu wa ziara hii, maelekezo yenyewe ni:
- 1- Watumishi wote wanaotoa huduma katika mawakibu wanatakiwa kuswali kwa wakati, na kila watu waswali mahala walipo, na hawatakiwi kutumia vipaza sauti na walinde heshima za njia.
- 2- Mawakibu (vikundi) vyote vya Husseiniyya vinavyo fanya maombolezo vitaingia kwa muda ulio pangwa, sawa viwe vya zainjiil au matam, vikundi vya zanjiil vinatakiwa kuingia mwezi 16 na 17 Safar, huku vile vya matam vinatakiwa kuingia mwezi 18 na 19 Safar.
- 3- Mawakibu zinatakiwa kukutana katika jukwaa la Aaridha lililopo karibu na mlango wa Kibla wa Haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa mujibu wa ratiba.
- 4- Mawakibu zitangia katika haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kutumia mlango wa Kibla na zitatoka kwa kutumia mlango wa Qaadhi haajaat, unao elekea upande wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, na wataenda kuingia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kisha wataondoka na kurudi katika maeneo yao.
- 5- Tunapenda kuwafahamisha watu wa Maukibu kua; hairuhusiwi kuimba Qaswida ndani ya haram mbili tukufu ya Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuchunga heshima na kulinda utulifu wa sehemu hizo takatifu.
- 6- Kiongozi wa Maukibu anatakiwa aonyeshe kibali alicho pewa kutoka ofisi ya polisi ya mkoa wa Karbala pamoja na kitambulisho alicho pewa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya cha Iraq na ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu.
- 7- Mkuu wa maukibu anajukumu la kulinda usalama wa watu wake, na anatakiwa kuzuia watu asio wajua kuingia katikati wa watu wake, atangulize watu wanao julikana watakao watambulisha watu wake kabla ya kuingia katika haram mbili tukufu.
- 8- Kuhakiki vipaza sauti na vitakaguliwa na watu wa usalama.
- 9- Hairuhusiwi kubeba siraha za moto na vifaa vyenye kukata pamoja na vifaa vya kubebea maji.
- 10- Hairuhusiwi kuonyesha picha yeyote ili kufanya tukio hilo kua linamuhusu Imamu Hussein (a.s).
- 11- Hairuhusiwi kufanya maigizo yasiyo beba ujumbe wa Arubainiyya, na ni lazima kuzingatia agizo hili, watakao fanya maigizo yasiyo sahihi watarudishwa waliko toka, kumbukeni kurejea kwa mateka na Imamu Sajjaad (a.s) kihistoria, hawakushindikizwa na majeshi ya baniy Umayya wala hakufungwa minrororo wala hawakupigwa.
- 12- Usinyanyue fimbo au bango lisilo nasibiana na maombolezo ya Arubainiyya.
- 13- Viongozi wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya watapewa vitabu vyenye maelekezo katika vituo vya ukaguzi vya nje na ndani ya mkoa wa Karbala.
- 14- Kuthibitisha sehemu itakapo kua Maukib ndani ya mji au nje kwa kiongozi mkuu wa uhusiano wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya.
- 15- Tunatarajia kuheshimiwa maelekezo haya, na kufuata ratiba iliyo pangwa na kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya pamoja na kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu na watoa huduma wa kujitolea bila kusahau vyombo vya ulinzi na usalama.
- 16- Ni marufuku kubeba vichwa au mizoga katika maigizo ya kuomboleza, na hata katika sehemu za Mawakibu, jambo hilo linashusha hadhi ya wahusika na halina maana katika mnasaba huu.
- 17- Mawakibu za maombolezo (dha’an) zinatakiwa kuingia mwezi 15 na 16 Safar.
- 18- Hairuhusiwi kuingia na ngoma kubwa, pia hairuhusiwi kupiga ngoma za aina zote ndani ya Ataba tukufu.
- 19- Kila maukibu inatakia kuweka kifaa cha kuzimia moto jikoni kwao ili waweze kuzuia haraka ajali ya moto kama ikitokea, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo.
- 20- Kuhifadhi mazingira ya barabara na mali za umma ikiwa pamoja na njia za maji, na kutofunga mahema juu ya njia au karo la maji, vile vile hairuhusiwi kutupa taka katika maeneo hayo, kwa ajili ya kulinda mtiririko wa maji.
- 21- Hairuhusiwi kutumia kuni wakati wa kupika, na unatakiwa kutumia gesi peke yake.
- 22- Hairuhusiwi kuchanganyika na wanawake katika maukibu (vikundi) nya kupiga matam na zanjiil.
- 23- Kuweka bango la utambulisho katika mlango wa maukibu (hema la kikundi) litakalo andikwa jina la kiongozi wa maukibu hiyo na namba zake za simu.