Miongoni mwa maandalizi yake katika ziara ya arubaini: Atabatu Abbasiyya tukufu yaonyeza vifaa vipya kwa ajili ya kuhudumia watu wanaokuja kufanya ziara..

Maoni katika picha
Idara ya kuhifadhi vitu na viatu iliyo chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa maandalizi ya ziara ya Arubainiyya imeongeza vifaa vipya vya kuhifadhia vitu vya watu wanaokuja kufanya ziara (mazuwaru), vifaa hivyo; vimewekwa katika eneo linalo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa nje pamoja na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Wameongeza vifaa hivyo ili kupunguza msongamano ambao hutokea katika ziara kubwa za mamilioni ya watu kama hii, vifaa vilivyo ongezwa ni kabati zilizo tengenezwa katika muundo wa vijisanduku, kila kisanduku kinaweza kuhifadhi vitu vya mtu mmoja, na kumfanya mtu huyo aende kufanya ziara akiwa hana wasiwasi wa usalama wa vitu vyake, kwani kila kisanduku kina ufunguo wake ambao umetengenezwa kwa umbo la saa ya mkononi atakao uchukua na kuuvaa, kila funguo imeandikwa namba ya sanduku lake, na kama ikitokea kwa bahati mbaya kapoteza ufunguo atamfuata mtumishi atakaye kua amekaa pembeni ya masanduku hayo na atapewa kopi nyingine ya ufunguo.

Kumbuka kua, kuwajali watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndio kipaombele kikubwa cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ndio maana inafanya kila iwezalo kuhakikisha inatoa huduma zote muhimu na kwa ubora mkubwa ili kumfanya zaairu ahisi amani na utulivu katika nafsi yake na kumuwezesha kufanya ibada kwa urahisi na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: