Tawi la uchapishaji na usambazaji la Darul-Kafeel lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho ya kimataifa ya (44) yanayo fanyika Bagdad linapata mwitikio mkubwa kila siku, jambo hili linaonyesha wazi kua watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya wanatilia umuhimu bidhaa vinazo onyeshwa na tawi hilo pia jambo hilo lina akisi maendeleo mazuri yaliyopo katika sekta ya uchapishaji.
Kiongozi mkuu mtendaji wa machapisho Ustadh Farasi Ibrahimiy ameelezea mazingira ya maonyesho haya na ushiriki wao, kwa kusema kua: “Maonyesho ya biashara sawa yawe ya kitaifa au kimataifa ni fursa nzuri ya kuonyesha bidhaa zinazo zalishwa na Darul-Kafeel miongoni mwa machapisho yake mbalimbali, hii ni mara ya tatu tunashiriki katika maonyesho haya, na kila mara inatofautiana na mara nyingine kutokana na kutofautiana kwa bidhaa tunazo onyesha”.
Akaongeza kusema kua: “Kitu cha pekee kwetu ni kwamba kila tunacho kionyesha kimetengenezwa Iraq (bidhaa halisi ya Iraq), tuna fahari kubwa kua na sisi ni miongoni mwa watu tunaochangia kurudisha heshima ya Iraq katika sekta ya viwanda”.
Kuhusu vitu wanavyo onyesha alisema kua: “Tunaonyesha nakala mbalimbali zilizo chapishwa na kituo chetu, kila moja inatofautiana na nyingine, pamoja na zile tulizo chapisha hivi karibuni kwa kutumia vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja na madaftari, hali kadhalika tumegawa folda (mikoba) ya utambulisho na kufungua kituo rasmi cha mauzo ya moja kwa moja, ikiwa kama sehemu ya kukiendeleza kituo hiki na kufungua mawasiliano na vituo vya usambazaji vya kitaifa na kimataifa itasaidia pia kujua maendelea katika sekta hii kimataifa”.
Kumbuka kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki wake wa maonyesho ya myaka ya nyuma, na kila mwaka hupata mwitikio mkubwa na wa aina yake, mwaka huu imeshiriki kwa kuwakilishwa na matawi matano, yanayo tengeneza bidhaa za viwandani, kilimo na chakula, ambayo ni: (Shirika la Nurul-Kafeel linalo zalisha bidhaa za wanyama, Shirika la Aljuud la teknolojia ya kilimo cha kisasa, Shirika la Liwaau Al-Aalamiyya la viwanda na biashara, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji pamoja na Shirika kuu la uzalishaji la Alkafeel lililo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji).