Chuo kikuu cha Ameed chaanza kupokea wanafunzi wanaopenda kujiunga katika michepuo yake kwa mwaka 2017 – 2018m.

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Ameed kilicho chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kupokea maombi ya wanafunzi wanao taka kujiunga katika michepuo yake ya (Udaktari, Udaktari ya meno na Uuguzi) kwa mwaka wa masomo 2017 – 2018m, chini ya kanuni na taratibu zilizo wekwa na wizara ya elimu ya juu katika vyuo binasfi.

Kila chuo kimeandaliwa sehemu maalumu ya kupokelea wanafunzi, na wameteuliwa wataalamu wa kujaza fomu za kwenye mtandao na kurahisisha shughuli ya usajili, usajili wa kujiunga na chuo hiki unafanyika katika mji wa Najafu, na chuo kipo katika mkoa mtukufu wa Karbala na kimesajiliwa kwa namba (1238).

Mkuu wa sheria katika chuo hicho Ustadh Ahmad Yaquub amebainisha kua: “Hakika chuo kimefungua milango yake na kupokea wanafunzi wanao penda kujiunga chini ya kanuni na taratibu za wizara ya elimu ya juu na utafiti, ambapo maombi ya kujiunga na chuo yanafanywa kwa njia ya mtandao na kupitia katika wizara ya elimu ya juu na utafiti, kiwango cha chini cha kukubaliwa katika mchepuo wa udaktari ni ufaulu wa (%93) na katika udaktari wa meno (%85) huku uuguzi ukiwa ni (65)”.

Akaongeza kusema kua: “Miaka ya nyuma wizara ya mambo ya nje iliruhusu kua na viwango sawa katika kupokea wanafunzi wa udaktari wa meno na uuguzi, kwa sasa chuo kinaweza kupokea wanafunzi (450) katika mgawanyo ufuatao: wanafunzi 100 mchepuo wa udaktari, 150 mchepuo wa udaktari wa meno na 200 uuguzi.

Akaendelea kusema: “Wanafunzi wanao taka kujiunga na chuo hiki wafanye haraka kuleta vielelezo vifuatavyo:

  • 1- Cheti cha sekondari chenye ufaulu tajwa hapo juu au uthibitisho kutoka katika uongozi wa malezi na elimu au shule uliyo somea. (nakala halisi).
  • 2- Kitambulisho chako cha uraia na vya wazazi wako (nakala halisi na kopi).
  • 3- Namba ya mtihani.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni taasisi ya kielimu iliyo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo idhinishwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti, imeanzishwa kwa lengo la kua kituo kikuu cha elimu, na inafuata vigezo na taratibu za kimataifa vitakavyo iwezesha kua miongoni mwa vituo bora vinavyo tegemewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: