Inatokea hivi sasa: Majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) waanza kutekeleza jukumu walilo pewa katika vita ya kukomboa mji wa Qaaimu na Raawah..

Maoni katika picha
Toka dakika ya kwanza ya kuanza awamu ya kwanza ya kukomboa mji wa (Qaaimu na Raawah), kama kawaida ya majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika kila vita, wameanza kutekeleza jukumu walilo pangiwa katika vita hii awamu ya kwanza, na wamefanikiwa kuwapa hasara kubwa adui zao ndani ya muda uliopangwa. Viongozi wa kikosi hicho wamesema kua; Idara ya upelelezi katika vita hii ya kukomboa miji ya magharibi ya Anbaar (Qaaimu na Raawah) inafanya jukumu lake kwa umakini wa hali ya juu na kutoa taarifa sahihi kwa wanajeshi wanao songa mbele, huku bruged ya wahandisi ikifanikiwa kutegua mabomu mengi yaliyo kua yametegwa barabarani kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Kumbuka kua asubuhi ya leo (Alkhamisi 5 Safar 1439h) sawa na (26 Oktoba 2017m) imeanza rasmi vita ya kukomboa magharibi ya Anbaar, ambayo ni ngome ya mwisho ya magaidi wa Daesh hapa Irag.

Na tunapenda kusema kua maandalizi ya kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita hii ni makubwa baada ya yale maandalizi waliyo fanya ya kukomboa mji wa Bashiri mwaka jana (2016m), inatarajiwa vita hii kua ya mwisho baada ya kupigana kwa miaka mitatu na miezi minne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: