Hivi ndiyo alivyo uawa kishahidi bibi Ruqayya bint wa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Vipindi vya msiba wa Imamu Hussein ni vingi, vinamzunguka mtu kila wakati, na vyote vinatia simanzi kabwa nyoyoni na macho kutoa machozi, ni kweli kusema wameangamia wasio lizwa na msiba wa Twafu na yaliyo jiri baada yake, miongoni mwa matukio yanayo huzunisha ni kuuawa kwa bibi Ruqayya bint wa Imamu Hussein (a.s), nyoyo za waumini hupata huzuni kubwa kutokana na msiba huo uumizao.

Hakika bibi Ruqayya (a.s) alishuhudia tukio la Twafu akiwa na umri wa miaka mitatu, akaona kwa macho yake kuuawa kwa baba yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na maswahaba zake, akachukuliwa pamoja na mateka wengine wa Ahlulbait (a.s) hadi katika mji wa Kufa, kisha wakapelekwa Sham.

Nafasi yake ilionekana zaidi alipo fika Damaskas kiribu na arshi ya madhalimu wa kibani Umayya, maneno yake (a.s) yalitikisha arshi ya baniy Umayya, yeye mwenyewe alitosha kua ujumbe wa haki mbele ya mfalme dhalimu, alikua akisema (Yuko wapi baba yangu… yuko wapi baba yangu) Mwenyezi Mungu ana shani yake ewe kipenzi changu uliyafanya haya ukiwa chini ya umri wa miaka minne.

Riwaya zinasema kua; wakati Ahlulbaiti (mateka) (a.s) walipo kua Sham, bibi Ruqayya alimuona baba yake katika usingizi, alipo amka akawa anasema: Yuko wapi baba yangu Hussein? Mimi nimemuona usingizini, wanawake walipo sikia maneno hayo walianza kulia na watoto wote wakaanza kulia pia, sauti za vilio zikawa nyingi, (mal-uni) Yazidi akaamka na akasema: Kuna jambo gani?

Akataka wamuambie kilicho tokea, nao wakamuambia. Akaamrisha apelekewe kichwa cha baba yake, walipo leta kichwa kitukufu na kukiweka miguuni kwake akasema: nini hii? Wakamjibu: kichwa cha baba yako. Alishikwa na butwaa akapiga ukulele akakumbatia kichwa kile (na akafariki hapo hapo) aliondoka (duniani) kwa utukufu na kaenda kumuambia babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na bibi yake Zaharaa (a.s) dhulma walizo fanyiwa..

Bibi Ruqayya bint wa Imamu Hussein (a.s) alifia Damaskas –Sham- Mwezi tano Safar mwaka (61) hijiriyya, akiwa na umri wa miaka mitatu au minne au zaidi ya hapo kidogo, na alizikwa sehemu ile ile aliyo fia. Muandishi wa kitabu cha Ma’aali Sibtwain anasema kua: “Hakika! Hashimiyya wa kwanza kufariki baada ya kuawa Imamu Hussein (a.s) ni mwanae bibi Ruqayya aliye fia Sham, kaburi lake tukufu lipo umbali wa mita mia moja au zaidi kidoga kutoka msikiti wa Umawiyya katika jiji la Damaskas, katika sehemu ya mlango wa Faradiis (Babu Faradiis), nao ni mlango mashuhuri na mkongwe sana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: