Wamefauli walio andika historia kwa nyayo zao, matembezi ya Arubainiyya..

Maoni katika picha
Wamefaulu walio andika historia kwa nyayo zao…

Wamefaulu wanaofanya matembezi yaliyo jaa upendo…

Hakuna awezae kuelezea ipasavyo, hongera yao wanaokata mawimbi mazito wakiwa na nyoyo zilizojaa mapenzi ya muokozi wa kuwatoa watu katika upotovu…

Hii ndio picha iliyo achwa na muhanga wa Imamu Hussein (a.s) na inaendelezwa na wapenzi wake katika kila zama.

Bado msafara wa Imamu Hussein (a.s) unaendelea, mkoa wa Basra na Dhiqaar inafanya matembezi yake ya milele kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika ziara ya Arubainiyya tukufu, na wanatangaza utiifu wao kwake katika bango ambalo halielezeki.

Kwa upande mwingine, Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyo toa huduma kwa mazuwaru wanao tembea kwa miguu kutoka Basra na Diqaar, vimejaa njia nzima na wanafanya kila wawezalo katika kutoa huduma kwa mazuwaru hao, wameandaa hadi vituo vya afya kwa ajili ya kutoa huduma za kimatibabu, na wamesambaza askari na wanajeshi wengi kwa ajili ya kulinda amani na usalama kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: