Kikosi cha Abbasi (a.s) chasonga mbele katika vita ya kukomboa magharibi ya Anbaar (Qaaimu na Raawah) na chafikia malengo kiliyo jiwekea..

Maoni katika picha
Kwa utukufu wa mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) ambaye tunatumia jina lake, kikosi cha Abbasi (a.s) kimepata mafanikio makubwa na kinasonga mbele katika vita ya kukomboa magharibi ya Anbaar (Qaaimu na Raawah), katika siku ya kwanza kikosi kimefanikiwa kudhibiti eneo lenye ukubwa wa zaidi ya kilometa (100), baada ya mashambulizi makali dhidi ya magaidi ya Daesh, na kilifanikiwa kukomboa kiwanda cha (90), na brugedi ya wahandisi ilifanikiwa kutegua makumi ya mabomu na kufungua njia kwa wapiganaji pamoja na kutegua mabomu yaliyo kua yametegwa katika magari.

Kiongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) amesisitiza kua; wapiganaji wanaendelea kusonga mbele na kupigana dhidi ya magaidi wa Daesh, na wameweka mpango maalumu wa kuwalinda raia na kuwahamishia katika maeneo salama.

Kumbuka kua maandalizi ya kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita hii ni makubwa baada ya yale maandalizi waliyo fanya ya kukomboa mji wa Bashiri mwaka (2016m), inatarajiwa vita hii kua ya mwisho baada ya kupigana kwa miaka mitatu na miezi minne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: