Mawakibu za kutoa huduma katika mkoa wa Basra ni vituo vya ukarimu..

Maoni katika picha
Mkoa wa Basra kama ulivyo kua toka zamani ukijulikana kwa utukufu na ukarimu, na umejitolea watu wengi kwa ajili ya kutetea uhuru na kulinda aridhi ya Iraq na maeneo yake matukufu, hali kadhalika unatoa huduma bora kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), watu wa mji huo wameonyesha kwa vitende mapenzi yao kwa Abul-Ahraar (a.s) kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwemo hii ya kuwahudumia watu wanao kwenda kuzuru haram yake tukufu, zinatolewa huduma za aina tofauti, kila mtu anatoa huduma kwa namna awezayo, kubwa zaidi ni kwamba njia zote kubwa na ndogo zimejaa watoa huduma.

Kwa mujibu wa shuhuda tulizo kusanya kuhusu huduma zinazo tolewa tumekuta kua ni kubwa sana na hazielezeki, na utawakuta watoa huduma wanashidhana katika hilo, na katika muonekano wa pekee kabisa unao onyesha ukubwa wa mapenzi yao kwa Imamu Hussein (a.s), na kufurahia kwao kumuhudumia mtu anaye kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s), kuna aina nyingi za huduma zinazo tolewa bure huku watoa huduma wakishindana katika ubora na wakionyesha furaha za nyoyo zao katika kujitolea kwao huko, wakiliwazika kwa kutoa huduma kanakwamba kuna kitu chochete wanacho lipwa na zaairu.

Kumbuka kua mkoa wa Basra ndio kituo cha kwanza katika aridhi ya Iraq unapo anzia msafara wa mazuwaru wengi zaidi kutoka ndani ya Iraq na nchi jirani, katika ziara hii wakazi wa mkoa huo hujitokeza kwa wingi katika kila kitongoji kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu wanao kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s), imekua ndio ada yao kila mwaka, shughuli hii huanza mapema na hufikia kilele chake mwezi sita na saba Safar, mawakibu na vikundi vya watoa huduma wameenea kila sehemu, watu wote utawaona wakishindana kutoa huduma, kwani huusubiri kwa hamu kubwa msimu huu wa ziara na hujiandaa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuja kutoa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: