Marjaa dini mkuu kupitia wakili wake Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi katika mimbari ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) amehusia kulinda mazingira ya ziara ya Arubaini.
Sayyid Swafi amebainisha kua: “Yapasa kulinda mazingira ya ziara, ili kupata mafanikio na faida tarajiwa katika ibada hii tukufu, na nyie mnafahamu wazi kua mazingira ya kipindi cha ziara yanatofautiana na mazingira ya kipindi kingine cha kawaida. Hakika mtu anapo mtegemea Mwenyezi Mungu na akakusudia kuja kumzuru Bwana wa Mashahidi (a.s), anatakiwa kulinda mazingira haya ya pekee katika ziara ya Arubaini, ili aweze kupata malipo mema anayo yatarajia kwa kuja kwake katika malalo ya Bwana wa Mashahidi (a.s)”.
Kumbuka kua Sayyid Swafi (d.i) ametaja mambo mengi katika khutuba hiyo aliyo husia kuhusu ziara ya Arubaini.