Muonekano wa njia ya peponi: Mtoto mwenye ulemavu aenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) na akataa kutumia kiti chenye mataili..

Maoni katika picha
Sajjaad mtoto mwenye miaka sita, mwenye ulemavu aliye lelewa Iraq na kuhisi uchungu wa damu iliyo mwagika katika vita ya Twafu, ameamua kwenda kufanya ziara kwa Imamu Hussein (a.s) kwa kutembea (kutambaa) na kukata mamia ya maili, kakataa kupanda mkokoteni (au kiti cha mataili), Imamu Hussein kwake ni mkubwa mno na hakutaka kwenda kwake akiwa juu ya kipando.

Wewe na watu wa mfano wako miongoni mwa wale wanaokuja wakiwa wamejaa machungu ya moto uliochama mahema, wanaelekea katika njia ya kuitafuta pepo wanatembea umbali mrefu kwa ikhlasi.

Ni mapenzi yaliyoje kwa Imamu Hussein! Kama yakiangukia katika jabali (jiwe) litapasuka?

Imani kubwa iliyoje imejaa katika nafsi zenu?

Wewe ewe Sajjaad pamoja na udogo wa umri wako lakini ni mkubwa kushinda maneno ya kukusifia, na ni mpana zaidi kuliko historia itakavyo kuelezea.

Pongezi kwako kwa maamuzi yako haya, hakika ni sifa kwa kila atakaye kuelezea, hakika Imamu wako Hussein (a.s) atakuombea shufaa mbele ya Mwenyezi Mungu na atamuomba akubadilishie miguu yako yenye ulemavu kua mbawa mbili zenye kupendeza hadi malaika wakuonee wivu.

Pamoja na kwamba umri wako haujafikia kuwajibikiwa na sheria lakini watu wa mfano wako huitwa mabwana, tunamuomba Mwenyezi Mungu akufikishe salama Karbala na urudi kwa watu wako ukiwa umenufaika, na ukubali ibada zako ewe mja uliye jitolea uhai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: