Ndani ya muda ulio pangwa: Kikosi cha Abbasi chakamilisha malengo yake ya awamu ya kwanza katika vita ya kukomboa magharibi ya Anbaar..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kukamilisha malengo yake katika vita wanayo shiriki ya kukomboa magharibi ya Anbaar (Qaaimu na Raawah) katika awamu ya kwanza.

Viongozi wa kikosi hicho wamethibitisha kukamilisha malengo yao ndani ya muda uliopangwa, na wamewapa hasara kubwa ya nafsi na mali magaidi ya Daesh, sasa hivi kikosi kinakusanya nguvu zake na kinasubiri awamu ya pili ya vita hiyo.

Katika awamu hii kikosi kimefanikiwa yafuatayo:

  • 1- Kukomboa zaidi ya eneo la kilometa 301.
  • 2- Kukomboa kiwanda cha Kasaraat cha Qaaimu.
  • 3- Kukomboa kiwanda cha (90) cha kuzalisha Fusfaat.
  • 4- Kukomboa kituo cha maji 70 Qaaimu.
  • 5- Kuangamiza magari matatu yaliyo jaa vilipuzi yaliyo lenga kukwamisha kusonga mbele wa wapiganaji wetu.
  • 6- Kutegua zaidi ya mabomu 100.
  • 7- Kudhibiti kituo cha mawasiliano kilicho kua kinatumiwa na magaidi wa Daesh.
  • 8- Kukomboa jangwa la Ukaashi, Uzaafi na Razaqah.

Kumbuka kua maandalizi ya kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita hii ni makubwa baada ya yale maandalizi waliyo fanya ya kukomboa mji wa Bashiri mwaka (2016m), inatarajiwa vita hii kua ya mwisho baada ya kupigana kwa miaka mitatu na miezi minne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: