Hakuna miongoni mwetu ispokua atauawa kwa panga au kwa sumu: Imamu Hassan (a.s) ni mfano..

Maoni katika picha
Siasa nzuri aliyo kua nayo Imamu Hassan (a.s) na heshima kubwa aliyo kawa nayo katika umma, vilisababisha Muawiya ashuku uwezo wake wa kupambana naye na kumzuia asikubalike katika umma, kwani Muawiya hakufanya jambo linalo pingana na sheria au maslahi ya umma ispokua Imamu (a.s) alimkosoa na umma wote ulimuunga mkono Imamu.

Njama zote za Muawiya zilifeli, akaamua kufanya hila nyingine, ambayo ni kukatisha uhai wa Imamu (a.s) kwa njia ya sumu.

Muawiya akamtuma mtu kwenda kwa mfalme wa Roma kutafuta sumu kali, Mfalme wa Roma akasema: Hakika sio halali katika dini yenu kumsadia mtu kumuua mtu asiye tushambulia.

Muawiya akamuandikia barua isemayo: Hakika mtu huyu (Imamu Hassan a.s) ni mtoto wa yule aliye taka kumuondoa baba yako katika ufalme (akikusudia, Mtume s.a.w.w) ndiye ninaye taka kumtilia sumu ili watu wasalimike naye na miji ipate amani.

Mfalme wa Roma akampa Muawiya sumu kali, Muawiya akampa Imamu (a.s) sumu hiyo kwa kumtumia Ju’dah, mke msaliti aliye tokana na familia ya watu waovu, baba yake alishiriki katika kumuua Amirulmu-uminina (a.s), na kaka yake alishiriki katika kumuua Imamu Hussein (a.s).

Baada ya kukaa siku arubaini toka alipo kula sumu (a.s) au siku stini, alikamilisha usia kwa ndugu yake Imamu Hussein (a.s), na akatambua kua kifo chake kimekaribia.

Akawa (a.s) anamuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: “Ewe Mola mimi naihesabu nafsi yangu kwako, hakika hili ni jambo kubwa kwangu, sijaona mfano wake, Ewe Mola liwaza kifo changu, na uniliwaze kaburini upweke wangu, hakika ni kweli -kaniwekea sumu katika kinywaji- (Muawiya) wallahi hajatekeleza alicho ahidi wala hakuna ukweli katika aliyo yasema”.

Akafariki (a.s) mwezi saba Safar mwaka wa 50 hijiriyya, na katika riwaya nyingine inasema ilikua mwezi 28 Safar mwaka wa 50 hijiriyya.

Watu wa Madina wakajitokeza kusindikiza mwili wa mtoto wa binti wa Mtume (s.a.w.w), aliye kua anakesha kwa ajili ya kutetea haki zao, na alikua anasimama kwa ajili yao wakati wote, msafara uliobeba mwili wake ukaelekea katika haram ya Mtume (s.a.w.w), ili wamzike karibu na kaburi la Mtume (s.a.w.w) na wahuishe utiifu wao kwake, kama alivyo husia Imamu mwenyewe.

Katika riwaya inasemekana kua: mikuki iliyo shambulia jeneza la Imamu (a.s), ilifika mikuki sabini, banu Hashim wakataka kupigana, Imamu Hussein (a.s) akasema: (Allah Allah, msivunje usia wa kaka yangu, hakika aliniambia kua; wakinizuia kumzika pembeni ya kaburi ya Mtume (s.a.w.w) nisigombane na yeyote, lau kama sio usia huo, mngeona namna gani ningemzika penmbeni ya kaburi la mtume (s.a.w.w)). Wakampeleka katika makaburi ya Baqii na wakamzika pembeni ya kaburi la bibi yake Fatuma bint Asadi (r.a).

Hivi ndio alivyo ishi mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), alikua na tabia nzuri, mtakasifu, muheshimiwa, mwenye kupendwa, na akafa shahidi, mwenye kudhulumiwa na mwenye kupewa malipo mema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: