Kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimetangaza kua; Mawakibu zinazo shiriki kutoa huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini mwaka huu zinakaribia (4000), maukibu (3000) zimekamilisha rasmi usajili, na zingine hazijakamilisha usajili, bado kuna vikundi vya Husseiniyya vingi vinavyo toa huduma pamoja na nyumba za watu binafsi ambazo zimefungua milango yao na kutoa huduma toka siku ya kwanza ya kuanza kwa matembezi ya ziara ya Arubaini, tena kuanzia kituo cha mbali huko Basra hadi katika mipaka yake na mikoa inayo pakana nayo, pia kuna maukibu zingine hufunga safari kutoka mbali na kuja Karbala kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu wanao kuja kufanya ziara.
Kitengo hicho kimesema kua; Mawakibu hizi zimeenea kila njia inayo pitiwa na mazuwaru, hususan maeneo yanayo pitiwa na mazuwaru wengi.
Wakabainisha kua: “Mwaka huu mazuwaru wanao tembea kwenda Karbala wameanza mapema, lakini mawakibu za kutoa huduma hazikubaki nyuma, wamefanya kazi kubwa ya kutoa huduma na kulinda usalama kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya mkoa, baada ya kumalizika misafara ya watembea kwa miguu katika mkoa huu wa Basra, vikundi vya mawakibu hufunga kazi zao, na wao huanza kutembea kwa kwenda Karbala ili wapate thawabu mara mbili za kutoa huduma na za kufanya ziara.
Kumbuka kua kiliundwa kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufanikisha shuguli hii, kinacho jumuisha watoa huduma watu wa usalama, vituo vya afya pamoja na viongozi wakuu wa mawakibu.