Uwepo wenye tija wa shirika la Liwaaul-Aalamiyya katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad..

Maoni katika picha
Miongoni mwa matawi yanayo shiriki katika maonyesho muhimu ya kimataifa yanayo endelea sasa hivi huko Bagdad ni shirika la Liwaaul-Aalamiyya linalo jihusisha na viwanda, biashara na uwakala wa kibiashara lililopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ushiriki wake katika maonyesho haya ya kimataifa umekua na tija kubwa, wasimamizi wa tawi hili wamehakikisha ushiriki wao usiwe wa kawaida, wamethibitisha uwepo wao kwa vitendo, kwa kuonyesha kazi zinazo endana na maendeleo ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya vifaa na umahiri wa watumishi wake, japokua limeanzishwa siku chache, wameweza kufikia malengo yao, yanayo endana na kinacho shuhudiwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa maendeleo makubwa katika sekta ya viwanda na ujenzi.

Wameonyesha sampo ya vitu vinavyo zalishwa na viwanda vyao, kama vile:

  • 1- Kiwanda cha kuzalisha kokoto za kujengea.
  • 2- Kiwanda cha kufyatua matofali na nguzo.
  • 3- Kiwanda cha kuchanganya zege.

Pia wamesambaza vipeperushi na kugawa mikoba (folda) zinazo elezea huduma wanazo toa.

Vitu walivyo onyesha vimepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu, mashirika na taasisi zilizo watembelea, hivyo umekua mwanzo mzuri wa kujitangaza kwa shirika hili, pia wamepata fursa ya kuangalia namna yanavyo fanya mashirika mengine ya aina hii ya kitaifa na kimataifa, ushiriki huu unasaidia kuongeza ufanisi wa kazi na kuangalia maendeleo yaliyopo katika sekta hiyo kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: