Kumrahisishia zaairu wa Arubaini: Kituo cha Alkafeel kinacho husu elimu na utafiti kimetoa ramani inayo onyesha njia kuu zote zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuwahudumia watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo matukufu ya Karbala, hususan wale wanao tembea katika msimu wa Arubaini, umefanyika utafiti wa kijografia wa kubaini njia kuu zote zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala.

Kituo cha Alkafeel cha elimu na utafiti katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha maandalizi ya ramani inayo onyesha njia hizo.

Haya yamesemwa na mkuu wa kituo hicho Ustadh Jasaam Muhammad Saidiy na akaongeza kusema kua “Katika ramani hiyo tumeonyesha vituo vya afya, usalama na maegesho ya magari ya muda, pamoja na maeneo ya kufanyiwa ziara, vibanda vya matangazo na sehemu kuu zinazo toa huduma, tumeainisha barabara kwa kuziwekea namba ili kumrahisishia zaairu aweze kufika kwa urahisi”.

Akabainisha kua: “Baada ya kukamilika uandaaji wa ramani ya mji wa Karbala na kuitafsiri katika lugha ya kiengereza ilipitishwa na ofisi ya mkuu wa mkoa”.

Akaongeza kua: “Kila kitu kimeainishwa katika ramani hiyo kwa mujibu wa vigezo halisi vya kijografia vilivyo fanyiwa uhakiki wa kina, kazi hii ilisimamiwa na kituo cha Alkafeel cha utamaduni na matangazo ya kimataifa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na walifanya kazi kwa kuwasiliana na idara ya Intanet na kuiweka ramani hiyo katika program ya mkoba wa mu-umin (Haqiibatul Mu-umin) katika usanifu mpya ulio fanyika hivi karibuni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: