Zaidi ya siku mbili, toka kuwasili kwa msafara wa mapenzi ya Husseini (Ishqu Husseiniyyu) unao kwenda kufanya ziara ya Arubaini kutoka Kuwait (Khaliij), msafara huo uliingilia lango la mtaa wa Fuhuud na wakaendelea na safari yao katika miji mingine.
Mkoa huo (Naswiriyya), unahistoria ndefu japokua unamazingira magumu, haujawahi kukubali au kunyenyekea dhulma, umeendelea kushikamana na Imamu Hussein pamoja na Ahlulbait (a.s) hata katika zama za utawala ulio pita (wa Sadam), uliowapa kila aina ya mateso, lakini waliendelea kuonyesha mapenzi yao kwa kutumia njia mbalimbali na wakajitolea uhai wao kwa ajili hiyo, pia wao ni wa kwanza kuitikia mwito wa Marjaa katika kila zama.
Wakazi wa Naswiriyya na mawakibu Husseiniyya pamoja na nyumba zote zilizopo katika njia inayo tumiwa na watu wanao enda kufanya ziara, wamewapokea vizuri sana mazuwaru na kuwapa kila aina ya huduma wanazo hitaji katika safari zao.
Kumbuka kua mikoa mingine ya kusini, Misaan, Diwaaniyya na Muthanna imeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru, tutaandika habari kamili baada ya kuwasili waandishi wetu waliopo huko.