Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo, Ustadh Muhammad Habibu Jibri, amesema kua: “Tumefanya hivi kutokana na malengo tuliyo jiwekea ya kuhakikisha tunafanya kila linalo hitajiwa na watu wanaokuja kufanya ziara kutoka ndani na nje ya nchi, ambao idadi yao inaongezeka kila siku kadri msimu wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) inavyo karibia, tumeandaa sehemu tatu zilizo chaguliwa kutokana na sehemu hizo kua na msongamano mkubwa wa watu, nazo ni:
- 1- Katika eneo la mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s) eneo linaukubwa wa mita (3000).
- 2- Katika eneo la uwanja wa Juud, eneo lenye ukubwa wa mita (200).
- 3- Katika eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad), eneo lenye ukubwa wa mita (250).
Akabainisha kua: “Maeneo haya ni makubwa, yanauwezo wa kuhifadhi maelfu ya mabeji, zimetengenezwa shelfu (kabati) zinazo endana na ukubwa wa kila eneo, tayali wamesha pangwa watumishi watakao kaa sehemu hizo muda wote, kila mtu atakaye hifadhi beji lake hapo atapewa namba maalum atakayo takiwa kuonyesha wakati wa kuchukua beji lake”.