Mashahidi wa Dhiqaar wawapokea mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Mawakibu (vikundi) vya watoa huduma katika mkoa wa Dhiqaar wamepamba barabara zao kwa picha za mashahidi walio jitolea nafsi zao takatifu kwa ajili ya kulinda nchi yao na maeneo matukufu, kila maukibu imeweka picha za mashahidi wake barabarani waliokua mstari wa mbele katika kuhudumia mazuwaru lakini Mwenyezi Mungu kapitisha uwezo wake na atakalo Allah ndilo hua.

Mkoa wa Dhiqaar ni sawa na mikoa mingine ya kusini, imemwaga damu nyingi kwa ajili ya kulinda taifa hili, watu wa mikoa hiyo walikua wa kwanza kuitikia wito wa Marjaiyya wa kuhami nchi yao na maeneo matukufu.

Mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi ndio taa zinazo angazia uhuru, damu ni utukufu wa shahidi na utukufu ni sifa ya taifa.

Mashahidi wetu ni kielelezo cha kauli mbiu ya Imamu Hussein ya; Uwe mbali nasi udhalili (Haihaata minna dhillah), hakika wao ni mashahidi waliofuata njia ya Imamu Hussein (a.s), ya kutafuta islahi na kulinda taifa na maeneo matukufu, na wameleta ushindi kwa damu zao takatifu.

Wamejitolea uhai wao kwa ajili ya nchi iitwayo IRAQ..

Hongera kwenu enyi mashahidi wa dini na utukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: