Kutokana na mkakati wa usalama makini, kitengo cha kutunza nidhamu chatangaza kujiandaa kwake kupokea mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Kitengo cha kutunza nidhamu katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kukamilika kwa maandalizi ya kuwapokea watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini, kutokana na umuhimu mkubwa wa kuhakikisha usalama katika ziara hii, watumishi wake hufanya kazi za ziada kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa mazuwaru watukufu, huratibu njia za kuingia na kutoka na kuweka vituo vya ukaguzi.

Makamo rais wa kitengo hicho, Ustadh Abdulhussein Habibu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maandalizi yetu katika ziara hii yamefuata maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, yanajumuisha kuandaa njia za kuingia na kutoka katika eneo la haram tukufu, hadi sasa tumesha sajili wafanya kazi wa kujitolea (700) ambao tutawaweka katika vituo vya ukaguzi vya nje na wengine katika milango ya kuingia katika eneo la haram tukufu.

Akaongeza kusema kua: “Watu wa kujitolea watafanya kazi ya kuratibu misafara ya watu sambamba na watumishi wa kitendo hiki na wataimarisha ulinzi katika vituo vya ukaguzi, pia kutakua na watumishi wetu watakao fanya kazi ya upelelezi katikati ya makundi ya watembea kwa miguu kwa ajili ya kuimarisha usalama katika eneo lote linalo zunguka haram tukufu na maeneo ya jirani na haram, pia kuchanganyika kwao na mazuwaru kutasaidia kutatua kwa haraka tatizo lolote linalo weza kutokea katikati wa watu kutokana na ukubwa wa msongamano, pia tutatumia mitambo ya kukagua mabeji (ID) katika vituo vyote vya ukaguzi, mitambo hiyo itawekwa maeneo yeto yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kitengo cha kutunza nidhamu kinafanya kazi kwa kushirikiana na idara ya mawasiliano ili kunufaika na sistim ya ulinzi kwa kutumia vioo (Screen) zilizo onganishwa na sistim ya kamera za ulinzi, mitambo hiyo inasaidia kudhibiti usalama na kubaini tatizo mapema pia kuweza kulitatua haraka kabla ya kutokea madhara makubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: