Ushuhuda katika njia ya pepo: Urefu mkubwa zaidi wa upangwaji wa chakula duniani washuhudiwa katika njia ya kwenda kwa Hussein (a.s) na kuweka rekodi mpya.

Maoni katika picha
Miongoni mwa ukarimu wako ewe Abu Abdillahi, mawakibu zaona fahari kufanya ukarimu, kwa nini isiwe hivyo wakati wewe ni ndugu wa Mkarimu wa Ahlulbait (a.s) Hassan Al-mujtaba (a.s), umelinda dini kwa nafsi yako na familia yako, wema na ukarimu hupatikana kutokana na imani, hawa hapa watoa huduma katika mkoa wa Dhiqaar, wanakuenzi ewe bwana wangu kwa kujitolea nafsi na mali zao, ili waingizwe katika historia ya utukufu, wanatandika chakula njia nzima kwa ajili ya watu wanaokuja kukuzuru na kuhuisha ziara ya Arubaini.

Watu wa mkoa wa Dhiqaar ambao wamezoea kugawa chakula kwa mazuwaru watukufu, wamepanga chakula cha aina mbalimbali njiani kwa urefu wa kilometa (75), wanashindana kutoa, kila mtu anatoa kadri ya uwezo wake, haijawahi kuripotiwa katika historia ukarimu na ugawaji wa chakula unaofikia hata nusu ya ukarimu wao, kwa sababu tukio la kuuawa kishahidi kwa mjukuu wa Mtume katika vita ya Karbala, na mazingatio yaliyo tokana na vita hiyo ni makubwa sana kushinda uwezo wa kawaida wa mwanadamu, hivyo utaendelea kua mkubwa mno utukufu wako ewe bwana wangu, hakika jua halijawahi kuangazia utukufu mkubwa zaidi kuliko huo, hongera sana kwa watumishi wa Hussein (a.s), hongera kwa kila anaye fuata mwenendo wake na hongera kwa atakae zuru kaburi lake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: