Msimamizi mkuu wa jambo hilo Shekh Twariq Bagdady amebainisha kua: “Hakika ziara ya Arubaini ya mwaka huu, itashuhudia kufanyika kwa kongamano la kwanza la (Msimu wa kitamaduni) chini ya usimamizi wa taasisi ya Qabsu Lithaqaafah wa Tanmiyya ikishirikiana na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na kushiriki jopo la wasomi kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq”.
Akafafanua kua: “Hakika huu ni mradi wa kwanza wa aina hii, unalenga kunufaika na mazingira ya kiroho yanayo patikana kwa mazuwaru, kwa ajili ya kutatua matatizo ya kijamii, kitamaduni, kimalezi na kifikra kupitia vituo vitakavyo funguliwa na mradi huu, ambavyo ni:
- - Kituo cha kulinda familia.
- - Kituo cha kutakasa tamaduni na tabia.
- - Kituo cha kusimamia vijana.
- - Kituo cha fani na adabu.
- - Kituo cha habari na athari zake katika jamii.
Shekh Bagdady akaongeza kusema kua: “Tunatarajia kua na matokeo mazuri katika kongamano hili, na kuweka msingi utakao tuwezesha kuifikia mikoa yote na kuunda kamati mbalimbali za vijana wenye uweledi na moyo wa kujitolea, watakao kufanya kazi katika sekta mbalimbali na miji tofauti baada ya msimu wa ziara”