Mawindo ya kamera ya Alkafeel katika matembezi ya wapenzi wa Hussein…

Maoni katika picha
Kamera ya Alkafeel imetembelea njia muhimu zinazo tumiwa na wapenzi wa Hussein wanao tembea kwa miguu, kufuatia ratiba iliyo wekwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na imeweza kuwaletea picha za mazuwaru na huduma zinazo tolewa na mawakibu za Husseiniyya kwa mapenzi makubwa yanayo tokana na kuwapenda Ahlulbait (a.s) kwa watu wanao kwenda kuhuisha viapo vyao vya utii kwa Abul-Ahraar (a.s).

Bado barabara za mikoa ya kusini hadi Karbala tukufu zinaendelea kujaa makundi ya watembea kwa miguu wakielekea katika Kaaba ya imani na kujitolea, aridhi ya Tufuuf inayo wakumbusha watu huru msimamo wa jihadi na kujitolea kwa Imamu Hussein (a.s), aliye jitolea nafsi yake na watu wa nyumbani kwake kwa ajili ya kutetea haki, uadilifu na usawa baina ya wanadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: