Ushuhuda katika njia ya pepo: Mtu anaye fanana na Abu Tahsiin na rafiki yake kipenzi atoa thawabu za kutembea kwake kwa shahidi huyo..

Maoni katika picha
Ameelekea Karbala akiwa na maumivu ya kumkumbuka kipenzi wake aliye kua akienda naye katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), Jemedari shujaa aliye hitimu katika shule ya harakati za Imamu Hussein (a.s) yeye pamoja na rafiki yake Abu Tahsiin, safari hii amekata masafa akiwa peke yake bila rafiki yake huku akiwa na machungu ya kumkosa.

Abu Karaar mpiganaji shujaa wa Hashdi Sha’abi, akiwa na majonzi makubwa ya kumpoteza rafiki yake Abu Tahsiin Swalehi, amekua kioo cha kila mwenye hamu ya kumuona mlenga shabaha Shahidi, ambaye hakupumzika toka ilipo tolewa fatwa na Marjaiyya, alijiunga na kikosi cha Ali Akbar na akuwa mpiganaji chini ya pendera ya Hashdi Sha’abi.

Shahidi Abu Tahsiin aliwapa maumivu makali magaidi wa Daesh kupitia bunduki yake, na alikua rafiki mkubwa wa Abu Karaar kuanzia katika vita ya Jurfa hadi Huweijah aliko pata utukufu wa shahada na kumuacha ndugu yake Abu Karaar akiendelea kumkumbuka katika njia ya kuelekea peponi, na akimzawadia thawabu za kutembea kwake kwenda Karbala.

Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Abu Tahsiin na amwandikie thawabu nyingi rafiki yako Abu Karaar, amkubalie ziara yake anayo fanya kwa niaba yako.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: