Kutoka katika idara za mpakani mwa mji wa Karbala: Zaidi ya maukibu 9000 va vikundi vya kutoa huduma wanashiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) miongoni mwake zipo za kiarabu na kiajemi..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) Haji Riyaadh Niimah Salmaan amesema kua; idadi ya mawakibu za maombolezo na utoaji wa huduma zinazo shiriki katika ziara ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu 1439 hijiriyya imefika (9450), kwa mujibu wa taarifa za mipakani mwa mkoa mtukufu wa Karbala, na zilizo orodheshwa rasmi, miongoni mwake zipo kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi, pia kuna mamia ya mawakibu ambazo hazija sajiliwa, pamoja na nyumba za makazi na madrasa ambazo zimefungua milango yao na kutoa huduma kwa mazuwaru.

Akaongeza kua: “Idadi ya mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vilivyo sajiliwa hivi karibuni imefika (1000) hii inamaanisha kuongezeka kwa idadi ya vikundi vya kutoa huduma kwa mazuwaru kunako endana na ongezeko la watu wanaokuja kufanya ziara katika kila mwaka”.

Akaongeza kusema: “Siku za nyuma tulifanya vikao vya maandalizi ya msimu wa Arubaini na wawakilishi wa mawakibu pamoja na viongozi wao, kwa ajili ya kuboresha huduma na kuendana na utukufu wa ziara hii pamoja na kutatua vikwazo, kitengo hiki kilitoa maolekezo na kanuni kwa viongozi na wasimamizi wa mawakibu, na tukatengeneza vitambulisho rasmi kwa kila maukibu na vikundi, tutateua watumishi wetu watakao tembelea maukibu hizo na kuandika taarifa zao za utekelezaji au uvunjaji wa maagizo yetu kama upo, pia watatembea sambamba na mawakibu za maombolezo na kuangalia kama wanatekeleza au wanakhalifu mambo tuliyo kubaliana, na watakao khalifu watafutwa katika ushiriki siku za mbele, pia wataratibu matembezi yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: