Zaairu wa Arubaini baina ya mapenzi ya Hussein na kumsubiri Mahdi..

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu kupitia khutuba ya pili ya swalaya Ijumaa, iliyo swaliwa leo (13 Shafar 1439h) sawa na (3 Novemba 2017m) katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), ikiongozwa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, amebainisha uhusiano wa zaairu wa Arubaini baina ya kumpenda Hussein na kumsubiri Mahdi, akaeleza kua:

Kwa namna gani tunaweza kudumisha misingi ya muhanga wa Imamu Hussein na njia sahihi vya kumsubiri Mahdi?

Na mambo gani yafanyikayo katika ziara ya Arubaini yanaweza kutuandaa kua na mapenzi ya dhati ya Imamu Hussein (a.s) na kua na nguvu ya mafungamano na Imamu wa Zama (a.f)?

Sisi kwa sasa –tupo katika zama za kusubiri- tuna mambo mawili, kumuamini Hussein (a.s) na kumuamini Mahdi (a.f).

Je! Inawezekana ziara ya Arubaini ikatufanikishia mambo hayo mawili: Kumpenda Imamu Hussein (a.s) na kufuata njia sahihi ya kusubiri, kuna tofauti baina ya zaairu wa Imamu Hussein (a.s) na mfuasi wa Ahlulbait (a.s), namna gani huyu zaairu ataweza kutumia ziara ya Arubaini apate mapenzi ya dhati kwa Imamu Hussein (a.s) na wakati huohuo afuate njia sahihi ya kusubiri? Kuna kusubiri kwa kweli na kwa uongo, kusubiri kuna nafasi gani na vitu gani vinavyo fungamana na kusubiri mbele ya Mwenyezi Mungu?

Kuna hadithi zilizo pokelewa kuhusu jambo hili yatupasa kutafakari maana zake, imepokewa katika hadithi kua: (Ibada bora ya Muumini ni kusubiri faraja) bila shaka kusubiri huku sio kwa kawaida kunako fanywa na watu wengi.

Hadithi nyingine inasema: (Atakaye kufa miongoni mwenu akiwa anasubiri jambo hili sawa na aliye kufa akiwa pamoja na Qaaimu katika nyumba yake).

Yatupasa kutafuta kiwango kipi cha subira kinacho takiwa kwa muumini hadi afikie daraja hili, tukiangalia kwa makini maana za hadithi tutaona kua; huyu Muumini mwenye kusubiri anatakiwa kua mfanya ibada mwenye ikhlasi na mwenye kumuamini Imamu Hujjah, na anaimani ya dhati ya kumsubiri na kajiandaa kua pamoja naye atakapo dhihiri Imamu Mahdi (a.s), atasimama pamoja naye, na kuungana na harakati zake, ni muelewa na anajua anacho kisubiri, ameandaa nafsi yake wakati wowote ule kusimama pamoja na Imamu Mahdi (a.f) na kumnusuru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: