Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya mahusiano Ustadh Azhar Rikaabiy, amesema: “Wanafunzi hawa kabla ya muda mfupi tulifanya makubaliano nao kwa kutumia wawakilishi wetu waliopo katika vyuo vikuu vya Iraq, tukawaomba washiriki katika utoaji wa huduma kwenye ziara ya Arubaini, na tulifanya nao vikao mbalimbali na kuwaelezea kazi watakazo fanya katika siku za ziara, kupitia vikao vivyo tuliwagawa kutokana na uhitaji wa vitengo vya Ataba, tuliwagawa katika maeneo yafuatayo:
- 1- Vituo vya wapotelewa.
- 2- Vituo vya uelekezaji.
- 3- Vituo vya afya.
- 4- Vituo vya upimaji wa afya.
- 5- Vituo vya huduma ya kwanza na magari ya wagonjwa.