Kikosi cha Abbasi cha vamia makao makuu ya mji wa Qaaim na chafikia malengo yake yote, chafika hadi kingoni mwa mto wa Furat

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kufikia malengo yake yote na kutekeleza jukumu kililo pewa, majemedari wa kikosi hicho wameweza kufika katika kingo za mto furat ndani ya muda ulio tarajiwa, wakiwa na wapiganaji wa kikosi cha Hizbu-Llah, baada ya kuwatimua magaidi wa Daesh katikati ya mji wa Qaaim.

Kikosi kimebainisha kua katika opresheni hii; wamekomboa mtaa wa Salaam na kitongoji cha (Karaabalah na makao makuu ya Qaaim) na wameangamiza idadi kubwa ya mahandaki pamoja na vilivyo kuwemo, ambayo walikua wakiyatumia maadui kuzuia kusonga mbele kwa vikosi vya ukombozi.

Kikosi cha mabomu na mizinga kilikua na mchango mkubwa ulio saidia kusonga mbele kwa vikosi vya ukombozi hadi katika makao makuu ya mji wa Qaaim.

Fahamu kua opresheni hii imefanywa kwa kushirikiana na ndege za kivita za jeshi tukufu.

Kumbuka kua maandalizi ya kikosi cha Abbasi (a.s) kwa ajili ya vita hii ni makubwa baada ya yale yaliyo fanyika kwa ajili ya kukomboa mji wa Bashiri mwaka jana (2016m), inatarajiwa hii kua vita ya mwisho baada ya kupigana miaka mitatu na miezi minne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: