Mkoa wa Dhiqaar zaidi ya maukibu Husseiniyya za kutoa huduma (2500) zimeshiriki katika kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Iraq na ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimetangaza kushiriki kwa maukibu zaidi ya (2500) katika kutoa huduma kwenye eneo la kijografia la mkoa wa Dhiqaar.

Maukibu hizo zimeenea kila barabara kubwa na ndogo inayo tumiwa na mazuwaru watukufu, idadi hiyo ni zile zilizo sajiliwa rasmi, bado kuna makumi ya mawakibu ambazo hazikusajiliwa pamoja na Husseiniyya nyingi zilizo fungua milango yake na kutoa huduma kwa watu wanao kwenda kufanya ziara.

Akaongeza kusema kua; kuna maukibu zimekuja kutoa huduma Karbala na zingine hutoa huduma katika mkoa wa Dhiqaar kisha huja kuendelea na kutoa huduma katika mkoa wa Karbala pia.

Watu wanaofanya kazi katika mawakibu za kutoa huduma, wanafanya kazi usiku na mchana bila kupumzika, wamejitolea mali na nguvu zao kwa ajili ya kutafuta thawabu za kumtumikia Hussein (a.s), pia maukibu hizo zinafanya kazi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi na kwa ufanisi mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: