Kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chaandaa utaratibu wa kusaidia kubeba mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi ya kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu ya kubeba mazuwaru wa Arubaini, ambalo ndio jukumu lake kuu, kimeandaa magari yenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kusaidia kubeba watu wanaokuja kufanya ziara pindi wanapo karibia katika mji mtukufu wa Karbala na wakati wakuondoka kwao.

Rais wa kitengo cha mitambo (magari) Muhandisi Abduljawaad amebainisha kua: “Swala la usafiri ni muhimu sana na linahitajiwa na watu wanaokuja Karbala katika ziara ya Arubaini, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru, tumejiandaa kukabiliana na hali hiyo kwa kukarabati na kuandaa idadi kuwa ya magari”.

Akaongeza kusema kua: “Kitengo chetu kitabeba mazuwaru kutoka na kwenda katika kituo cha Qantwara Salaam upande wa mkoa wa Baabil (Stendi ya Ummu Hawaa) ambayo inamsongamano mkubwa wa watu”.

Akabainisha kua: “Tumeandaa zaidi ya gari 150 za ukubwa tofauti, pamoja na magari maalum, kama vile gari za wagonjwa, kituo chetu kikuu itakua hapohapo stendi kwa ajili ya kutia mafuta na kupumzika (kupokezana) madereva, kwani kazi hii itafanyika saa zote (hakuna kupumzika), pia tumeandaa gari za doria kwa ajili ya kufanya matengenezo ya haraka kwa gari yeyote itakayo haribika katikati ya safari”.

Akaendelea kusema kua: “Hali kadhalika tumeandaa gari kubwa 150 zilizo tolewa na kikosi cha jeshi la muungano na gari zingine 50 zimetolewa na wakazi wa kijiji cha Haswiin kilichopo Hilla kama sehemu yao ya kusaidia sekta ya uchukuzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: