Tangazo la kuanza rasmi kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini: Jumuiya ya Scaut ya Alkafeel yapandisha bendera ya kutoa huduma..

Maoni katika picha
Jumuiyya ya Scaut ya Alkafeel iliyo chini ya idara ya watoto katika Atabatu Abbasiyya tukufu yajiandaa kutoa huduma kwa watu wanao kuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika maeneo ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa maeneo hayo ni: (Majengo ya Ummul-Banina, (a.s), majengo ya Alqamiy na majengo ya Shekh Kuleiniy q.s).

Kiongozi wa idara ya watoto na makuzi Ustadh Sarmad Salim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Wamefanya maandalizi makubwa kutokana na ukubwa wa kazi watakazo fanya, na wamegawanywa katika vikundi, kila kundi limepangiwa jukumu maalumu tofauti na kundi lingine”.

Akaongeza kua: “Juma Tano iliyo pita ilipandishwa bendera ya utoaji wa huduma katika hafla maalumu iliyo funguliwa kwa Qur’an tukufu na kuhudhuriwa na makamo katibu mkuu Sayyid Naafii Mussawiy pamoja na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu dokta Abbasi Didah, pamoja na jopo la mashekhe watukufu wakiwemo viongozi na wajumbe wa Jumuiyya hiyo, na wakaanza rasmi kutoa huduma kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi (a.s) walio kuwepo katika eneo la majenge ya Ummul-Banina (a.s)”.

Akaongeza kua: “Kulikua na muongozo uliotolewa kwa wana Scaut na baada yake wakaimba wimbo wa kuomboleza watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kisha wakaonyesha igizo na mwisho ikapandishwa pendera.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: