Ukiwa Muiraq hiyo ni kheri kwako kwani utapata utukufu na haiba nzuri kutoka katika malalo ya Sayyid Shuhadaa Imamu Hussein (a.s).
Utakapo kusudia kwenda Karbala kwa kutembea utaona fahari namna wananchi wa Iraq walivyo shikamana na kuongea lugha moja ya Hussein (a.s).
Hata ukitoka katika mji wa mbali kabisa utawakuta wairaq wanatoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wa ndani na nje ya Iraq.
Utaona utukufu zaidi na haiba kubwa unayo pata kutokana na Hussein, pale mamilioni ya watu wanapo shindwa kuelezea shukrani zao kwa raia hawa wa Iraq, hadi baadhi yao wameamua kuandika katika beji na nguo zao kua wanatoa shukrani zisizo na kifani kwa raia wa Iraq.
Hongora kubwa kwa Iraq, aridhi yake imehifadhi miili ya manabii na mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein (a.s), ambaye amekua kibla ya kila mtu huru duniani, huja kutembelewa na mamilioni ya watu kila mwaka hususan katika ziara ya Arubaini, kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu, pili tunamshukuru Imamu Hussein (a.s) kwa neema hii.
Kama sio wewe ewe Hussein tusingekua na ubora wowote mbele ya walimwengu, lakini sasa walimwengu wanatupa heshima kwa sababu tunajaribu kuonyesha ukarimu wako katika ziara, na kuonyesha ujemedari wako katika vita ambayo tumefanikiwa kukomboa miji iliyo kua imetekwa na magaidi.