Harakati kubwa ya usomaji wa Qur’an kwa wanawake wakati wa utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Vituo vya usomaji wa Qur’an katika njia zinazo elekea Karbala tukufu havija ishia upande wa wanaume peke yake, hata upande wa wanawake kumekua na harakati kubwa ya usomaji wa Qur’an.

Mkuu wa wanawake wanao shiriki katika vituo vya usomaji wa Qur’an Ustadhat Amal Maturiy amebainisha kua: “Wasomi wa Qur’an wanao shiriki katika mradi wa vituo vya usomaji wa Qur’an katika ziara ya Arubaini, vilivyo kila mkoa unao tekeleza mradi huu vipatavyo (100), vimeenea kila njia inayo tumiwa na mazuwaru watukufu, mradi huu inalenga kunufaika na vipawa vya usomaji wa Qur’an vya wakina mama, na umewekwa utaratibu wa kuwashirikisha wanawake wanao kwenda kufanya ziara kwa kuwafundisha usomaji sahihi wa Qur’an pamoja na mambo mengine”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika vituo vya usomaji wa Qur’an vya wanawake vipo katika mikoa 12, kuanzia mkoa wa Basra hadi Karbala tukufu, vituo hivyo vinazungukiwa na wanawake wasomi wa Qur’an kutoka katika Ataba tukufu na Mazaru takatifu na wengine wametoka katika taasisi za Qur’an zilizopo chini ya muungano wa jumuiya za Qur’an hapa Iraq”.

Kumbuka kua wasomi wa Quran wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu na mazaru, wamesha wahi kufanya mikutano ya kujadili namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano na kufanikisha mradi huu katika ziara ya Arubaini, unao simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na mazaru takatifu kwa kushirikiana na muungano wa jumuiya za Qur’an hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: