Pamoja na tabu wanazo pata kutokana na vimbunga vya vumbi na mvua lakini wana sura za bashasha na nyoyo imara zinazo funika uchovu wa miili yao katika kuwahudumia watu wanao kwenda ziara.
Hivi ndio wanavyo huisha ziara ya Arubaini kwa kutembea kwa miguu watu wa mji wa Diwaniyya na miji mingine ya Iraq.
Mji wa Diwaniyya upo kilometa 180 kusini ya mji wa Baqdadi na huchukuliwa kama lango kuu la watu wanao kwenda Karbala kwa kupitia njia ya Hilla au Najafu.
Hupokea mamilioni ya watu wanaotoka katika mikoa ya kusini wakiwa pamoja na watu wanaotoka katika nchi jirani, na hapo ndio mapanda njia, baadhi yao huelekea Najafu kisha Karbala na wengine huenda Baabil kisha Karbala kutekeleza ibada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), mkoa huu bado unaendelea kupokea na kuaga misafara ya mazuwaru, kupitia maukibu nyingi za kutoa huduma ya chakula, vinywaji na matibabu, pamoja na maukibu hizo pia nyumba nyingi zimefungua milango yao na kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu.
Hivi ndio wanavyo hudumiwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), wanaguswa na kauli ya Imamu wao Swadiq (a.s) alipo sema: Ewe Mola! Zirehemu nyuso zilizo badilika kwa jua… na uyarehemu macho yaliyo toka machozi kwa ajili ya kutuonea huruma… na urehemu nyoyo zinazo tupenda, na urehemu sauti iliyo toka kwa ajili yetu.