Ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), imechangia sana kujenga mshikamano na umoja wa wairaq na uwezo wao wa kusimama imara wakati wote na kuto kukubali kushindwa na tatizo, au njama za magaidi wanao tafuta kila njia ya kuishambulia Iraq na kuifanya kua nchi dhaifu yenye mipasuko, wakati wairaq wameshikamana katika misingi ya Mwenyezi Mungu na wana maelewano yaliyo komazwa na damu ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), na kauli mbiu yao inasema (Uwe mbali nasi udhalili), kauli hiyo huikariri wanapo patwa na mitihani au balaa zenye kuumiza.
Hakika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) sio lele mama, imetoa somo na kuwaandaa wairaq katika kupambana na mitihani na matatizo, upambanaji wa wairaq dhidi ya magaidi wa Daesh ni dalili ya wazi ya hili tunalo sema, waliweza kuharibu njama za magaidi zilizo lenga kuharibu taifa lao na kuvunja umoja pamoja na kuharibu muelekeo wa nchi kwa sasa na baadae.