Katika Atabatu Abbasiyya tukufu hakuna kitengo ambacho hakija husika na kutoa huduma ya moja kwa moja kwa mazuwaru wa Arubaini, bali kuna vitengo vinafanya kazi kwa ajili ya kuchangia na kutafuta thawabu, miongo mwa vitengo hivyo ni Dalul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji.
Kitengo hiki kimefanya kazi kubwa sana, watumishi wake wamefanya kazi kwa muda mrefu ya kuchapisha pipeperushi karibu milioni, ambavyo ni: (folda, vijitabu, brushua na cd), vilivyo jaa maelekezo, nasaha za kidini, hukumu za kisheria, kifiqhi na ki-aqida pamoja na ramani zinazo muongoza mtu aliye kuja kufanya ziara ya Arubaini, pia vina ziara tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), vikiwa katika lugha mbalimbali (Kiarabu, Kiingereza, Kifarsi na Kiswahili).
Katika uchapishaji wa vipeperushi hivi, tumezingatia sifa nyingi za uchapishaji, ikiwa ni pamoja na ubora wa wino, karatasi, muonekano wa maandishi na vinginevyo kutokana na utukufu wa ziara hii.