Muhimu sana kwa zaairu wa Arubaini.. njia ya kukutana walio potezana..

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nao ndio wahusika wakuu wa vituo vya waliopotelewa, Muhandisi Abbasi Hamza, amebainisha njia itakayo saidia kupata kitu kilicho potea ua mtu aliye potea, kwa kuripoti katika kituo cha karibu cha kuongoza walio potea na kutunza vilivyo okotwa, vilivyo enea kila kona ya mji mtukufu wa Karbala, upande wa mkoa wa Baabil, Najafu na Bagdad.

Kabainisha kua: “Vituo vipo (30) vimeunganishwa program yenye fomu maalumu, inayo ingizwa maelezo ya aliye potea au anaye tafuta (jina, umri, anuani, rangi za nguo na mengineyo) baada ya kuingiza maelezo hayo inakua rahisi kutambua alipo mtafutwaji”.

Akaongeza kua: “Kama hakuna maelezo ya kutosha kuhusu mtu aliye potea, tutatumia kipaza sauti kutangaza, ambapo sauti itasikika katika vituo vyote na itakua rahisi kumpata na atahifadhiwa hadi akutane na ngugu yake au mtu wake wa karibu”.

Muhandisi Faras akaendelea kusema kua: “Baada ya kupatikana atajulishwa ndugu yake kwa kutumia simu ya mkononi na atapelekwa na watumishi wetu walio enea kila kona hadi sehemu ndugu yake alipo, na atakabidhiwa baada ya kuthibitisha uhusiano wao, kama aliye potea yupo mbali na wenzake tutamuandalia usafiri wa kumpeleka kwa wenzake, na tutatumia mbinu ileile ya kuthibinisha uhusiano wao kwanza ndipo tunamkabidhi kwao”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Hakika vituo hivi vimeunganiswa na chumba cha ukaguzi cha Atabatu Abbasiyya tukufu na vinafanya kazi saa 24, kwa kuwasiliana na vituo hivi au unapo taka kutoa taarifa yeyote unaweza kupiga namba zifuatazo:

07602405888

07602405889

Pamoja na kutaja sehemu ulipo na kituo cha karibu na maha ulipo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: