Ushuhuda kutoka katika njia ya kuelekea peponi: Haidari na Aqiil walipoteza macho yao lakini muono wao wa moyoni unawaongoza njia ya kwenda kwa Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Haidari na Aqiil wamemuona Hussein kwa nyoyo zao bila vunmbi, na wakaona njia ya kwenda kwa Hussein na wakaifuata, wamemtambua Hussein hawajampotea, walipoteza macho, hawaja poteza kuona, uwezo wa Mwenyezi Mungu unawawezesha kuwaona wapenzi wao kwa kutumia nyoyo, bali nyoyo zao ni nuru.

Haidari na Aqiil ni wakazi wa Faau wenye ulemavu wa macho, ni marafiki ambao kila mwaka huenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Hussein (a.s), kama Jaabir (r.a) alipoteza macho na akaenda kwa Imamu Hussein (a.s), katika zama hizi kuna waja wema wanao msubiri Mahdi (a.f) kama alivyo kua Jaabir.

Haidari ana umri wa miaka (40) na Aqiil miaka (35), wanapita njia isiyo kua na watu wengi kuelekea Karbala ili wasiwakere watu wengine kutokana na udogo wa mwendo wao.

Haidari na Aqiil wanatembea pekeyao bila kua na muongozaji wa njia, jambo hili limemshangaza kila aliye sikia habari yao, wanasahau kua wao ni waumini, vipi bibi Khadija mama wa waumini awaache wanawe bila kua na wakuwaongoza, vipi bibi Zaharaa asiwapokee wageni wake, vipi wawe bila muongozaji wakati mikono ya Abulfadhil imewakumbatia wairaq.

Kitu gani kitasemwa kwa watu kama nyie? Kitu gani kiandikwe kuhusu nyie? Kalamu zinashindwa kuandika enyi watu wenye uoni, amani iwe juu ya nyoyo zenu zionazo, Mwenyezi Mungu akufikisheni Karbala mkiwa salama na mrudi mkiwa na mafanikio, mmekubaliwa ziara yenu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: