Hakika kwenda unatembea kwa Imamu Hussein (a.s) unapata thawabu tofauti na kwenda ukiwa umepanda, hii ni wakati wote na kila tukio maalumu la ziara ya Hussein (a.s).
Kutoka kwa Abu Swaamit anasema: Nilimsikia Abu Abdillahi (a.s) anasema: (Atakaye kwenda katika kaburi ya Imamu Hussein (a.s) akiwa anatembea, Mwenyezi Mungu atamuandikia kwa kila hatua thawabu elfu moja na atamfutia dhambi elfu moja na atampandisha daraja elfu moja).
Na katika riwaya nyingine kutoka kwa Abu Saidi Alqaadhi anasema: Niliingia kwa Abu Abdillahi (a.s) nikamsikia anasema: (Atakaye kwenda katika kaburi ya Hussein (a.s) akiwa anatembea, Mwenyezi Mungu atamuandikia kwa kila unyayo thawabu za kumuacha huru mtumwa katika kizazi cha Ismail). Angalia kitabu cha Kaamil ziyaraat ukurasa wa 255 – 257).
Kisha kuna umaalumu wa pekee (khususiyya) katika ziara ya Arubaini, hakika kutembea hadi Karbala, pamoja na fadhila zilizo tajwa, pia ni sehemu ya kuomboleza familia ya Hussein (a.s) iliyo pata maumivu na mateso (ya kutembea) hadi walipo fika kwa Imamu Hussein (a.s) katika siku ya arubaini, mpenzi wa Hussein (a.s) huhisi machungu na mateso waliyo pata familia ya Hussein (a.s).