Ratiba maalumu ya mawakibu za maombolezo (zanjiil) katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), kimetangaza ratiba ya uingiaji wa mawakibu za maombolezo (zanjiil) zinazo shiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambapo zimepangiwa siku mbili (mwezi 16 na 17 Safar).

Wakasisitiza kua: “Muda ulio pangwa; ni kuanzia kuondoka katika jukwaa lililopo karibu na Aaridha katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), kisha kuingia katika Atabatu Husseiniyya tukufu halafu kuelekea katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kumaliza maukibu (matembezi), yawalazimu viongozi wa mawakibu na vikundi vyote vya Husseiniyya kutoka mikoa yeto ya Iraq kuheshimu muda uliopangwa”.

Kitengo cha wenye mawakibu kimetoa wito kua: “Watumishi wote wa Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru watukufu asipatikane atakaye halifu ratiba hii”.

Mwezi 16 Safar 1439h:

 • 1- Mkoa wa Naswiriyya wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
 • 2- Mkoa wa Badgad wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa tano adhuhuri.
 • 3- Mkoa wa Najafu wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 7 baada ya adhuhuri hadi saa 8 baada ya adhuhuri.
 • 4- Mkoa wa Diwaniyya wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 8 baada ya adhuhuri hadi saa 10 alasiri.
 • 5- Mkoa wa Misaan wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 10 jioni hadi saa 11:30 Jioni.
 • 6- Kadhimiyya tukufu, kuanzia saa 1 jioni hadi saa 2 jioni.
 • 7- Mkoa wa Diala, kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.
 • 8- Mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 usiku.

Mwezi 17 Safar 1439h.

 • 1- Mkoa wa Basra wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
 • 2- Mkoa wa Baabil wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 asubuhi.
 • 3- Mkoa wa Waasit wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 7 baada ya adhuhuri hadi saa 9 alasiri.
 • 4- Mkoa wa Karkuk na Nainawa wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 9 baada ya adhuhuri hadi saa 10 alasiri.
 • 5- Mkoa wa Swalahu-Dini wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 10 jioni hadi saa 11:30 jioni.
 • 6- Mkoa wa Samawa wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 1 jioni hadi saa 2 usiku.
 • 7- Mkoa wa Naswiriyya wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.
 • 8- Mawakibu kutoka katika nchi za kiarabu na kiislamu saa 4 usiku hadi saa 6 usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: