Bado kamera za kituo cha uzalishaji cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinaendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika matembezi ya watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wameanzia mbali kufuatana na msafara huo hadi kufika katika mkoa mtukufu wa Karbala, wameweza kurusha picha bora zikiambatana na mahojiano waliyo fanya na mazuwaru.
Kiongozi wa kituo hicho Ustadh Bashiri Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kamera bado zinaendelea kupiga picha kwa kufuata ratiba maalumu iliyo pangwa, na tumewapanga vijana wenye utaalamu na sekta hiyo, wamethibitisha umahiri wao kwa kutuletea picha zinazo onyesha hali halisi ya kinacho endelea katika matembezi hayo pamoja na huduma zinazo patikana katika matembezi hayo, na wameweza kuzionyesha katika nchi nyingi za duniani tena zikiwa na ubora mkubwa, (kwa kutumia masafa ya bure bila kutumia masafa ya ndani)”.
Akasisitiza kua: “Masafa hiyo imenufaisha makumi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq kwa sababu inaendana na urushaji wao wa matangazo”.
Akaongeza kua: “Matangazo hayajaishia kuonyesha matembezi ya mazuwaru peke yake, bali kuna matangazo mengine yanayo endelea ndani ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Na mwisho ametoa wito kwa vyombo vyote vya habari vinavyo taka picha na matukio ya ziara hii kutumia anuani zifuatazo:
Satellite: Intelsat 902
Degree: 62e
Dl:11458V
SR:3000
Mod:DVBS-2
FEC:5/6
HD/MPEG-4
Matangazo yanarushwa kwa ratiba ifuatayo:
Matangazo ya kila siku kuanzia saa 2:00 asubusi hadi saa 5:00 asubuhi, na kuanzia saa 7:30 mchana hadi saa 10:30 jioni.
Masafa maalumu zinazo tumika kurusha matukio ndani ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ni hizi zifuatazo:
Sat E3B@3°E
Dl:11471.7 V
SR:2500
Mod:DVBS-2
FEC:5/6
HD/MPEG-4
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Ustadh Bashiri Taajir kiongozi wa kituo cha uzalishaji cha Alkafeel kwa kutumia namba za simu: (009647706007187) au wasiliana na Muhandisi Ihabu Awidi kiongozi wa idara ya uzalishaji katika Atabatu Abbasiyya kwa namba ya simu: (009647706054144).
Vyombo vya habari ambavyo haviwezi kutumia anuani hizo, kituo kimefungua kurasa katika mitandao ya kijamii, (facebook) anuani ifuatayo:
https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Na (youtubu) anuani ifuatayo:
https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw